BARAZA LA WANAWAKE WA CHADEMA (BAWACHA) MKOA WA RUVUMA WAMEMUOMBA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA KUTENGUA UTAUZI WA ZUBEDA HASSAN SAKURU KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA RUVUMA
Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa
wa Ruvuma wamesema wanapinga vikali kuteuliwa Zubeda Hassan Sakuru kuwa Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.
Wanachama wa BAWACHA Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma wametoa Tamko la pamoja, wapo tayari kutoka CHADEMA endapo uteuzi huo hautabatilishwa wamesema Zubeda Hassan Sakuru siyo mkaazi wa Mkoa wa Ruvuma hata wilaya waliyo sema ana toka Tunduru hakuna hata mmoja anaye mjua . Jambo waliyo baini nikuona chama kipo mkononi mwa mtu mmoja.
Wanawake wa CHADEMA kutoka wilaya za Tunduru, Nyasa, Mbinga, Namtumbo, Songea Vijijini na Songea Manispaa walipokutana katika Ofisi za CHADEMA wilaya ya Songea kutoa TAMKO hilo.
Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Ruvuma (BAWACHA) wakiwa ndani ya Ofisi za CHADEMA wilaya walipokutana kwa ajili ya kutoa tamko la kupinga Uteuzi wa Mbunge wa Viti Maalum atakayewakilisha Mkoa wa Ruvuma uliofanywa na Uongozi wa CHADEMA Taifa.
wanachama wa Chadema wakiwa nje ya Ofisi za CHADEMA wilaya Matarawe Manispaa ya Songea mara baada ya kutoa Tamko la Kupinga Uteuzi huo wa Mbunnge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.
Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma (BAWACHA) wamemuomba
Mwenyekiti wao wa CHADEMA Taifa Filiman Mbowe kubadilisha uteuzi alioufanya
kumteua mtu ambaye hayuko katika Mkoa wa Ruvuma anaye tokea Tanga na kumteua
kama mkazi wa Mkoa wa Ruvuma.
Wanachama wa BAWACHA nje ya Ofisi za CHADEMA wilaya ya Songea Mjini.
Wanawake wa Mkoa wa Ruvuma wa Chama cha CHADEMA wametoa siku
tatu kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Filiman Mbowe kutengua Uteuzi wake wa
kumuweka Zubeda Sakuru kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma wakati yeye
ni Mwenyeji wa Mkoa wa Tanga na Ushahidi upo wa yeye kugombea Mkoa wa Tanga.
Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma
wameshangaa kuona hata Uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma hawakuonekana katika kikao
kilicho andaliwa rasimi kupinga uteuzi wa Zubeda Sakuru na kudai uteuzi huo
wa kumfanya Mbunge wa mkoa wa Ruvuma wamedai
umetumika kulipa fadhila zinazo tiliwa mashaka.